#Local News

SERIKALI YAKAZA KAMBA DHIDI YA KLINIKI NA SPA ZINAZOFANYA UPASUAJI HARAMU

Wamiliki wa kliniki za urembo na SPA ambazo ufanya upasuaji kinyume cha sheria wamejipata taabani baada ya wizara ya afya kuanzika msako mkali dhidi yazo Katibu wa Afya ya Umma, Mary Muthoni, amesema tathmini ilifanywa katika maeneo ya Nairobi, Mombasa, Nakuru, na Eldoret.

Kati ya kliniki 26 zilizokaguliwa, 20 zilikuwa na leseni halali, tatu zilikuwa kwenye mchakato wa usajili, huku tatu zikifanya kazi bila usajili. Pia, spa 102 zilifanyiwa ukaguzi, ambapo saba zilipatikana zikitoa huduma hatari kama micro-blading na micro-needling bila usajili au wahudumu wenye ujuzi.

Muthoni amesema kuna haja ya utekelezaji mkali wa sheria na uhamasishaji wa umma kuhusu hatari za huduma zisizo salama. Amewataka wamiliki wa biashara za urembo kuzingatia sheria ili kuhakikisha usalama wa wateja.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *