SERIKALI MBIONI KUIMARISHA AFYA YA AKILI

Visa vya matatizo ya afya ya akili vinatarajiwa kupungua baada ya wizara ya afya kuzindua mwongozo wa kwanza wa kliniki kwa lengo la kudhibiti visa hivyo kwa kuimarisha upimaji na matibabu kwa waathiriwa. Mkuu wa idara ya afya ya familia Bashir Isaak amesema mwongozo huo unalenga kushughulikia mwanya wa asilimia 75 katika huduma za kimatibabu […]

LENGO LA KUMBANDUA GAVANA WA NYAMIRA AMOS NYARIBO LATIBUKA

Wawakilishi wadi wa bunge la kaunti ya Nyamira wamefichua nia yao ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na uongozi wa gavana wa kaunti hiyo Amos Nyaribo. Hatua hii inajiri baada ya spika wa kaunti hiyo Enock Okerokuithinisha ombi la kuwasilisha rasmi hoja hiyo leo mwendo wa saa nane. Hoja ya kumbandua gavana huyo inafathiliwa […]

ALIYEKUWA MPENZI WA MWANARIADHA REBECCA CHEPTEGEI DICKSON NDIEMA AMEFARIKI

Aliyekuwa mpenzi wa mwanariadha Rebeca Cheptegei Dickson Ndiema ameaga duniaHospitali ilithibitisha kuwa Ndiema amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) alikokuwa amelazwa. Ndiema amefariki siku chache baada ya Cheptegei kufariki katika hospitali hiyo hiyo.Ndiema alimvamia Cheptegei nyumbani kwake ambapo alimmwagia petroli na kumchoma moto ambao pia ulimjeruhi. Imetayarishwa na Janice Marete

WASHUKIWA WAWILI WA KESI YA MAUAJI YA SIAYA KUWA MASHAHIDI WA SERIKALI

Jean Ogol, mwalimu wa shule ya msingi na Henry Opiyo, waliokamatwa kuhusiana na mauaji ya mzee wa miaka 40 huko Bondo, Kaunti ya Siaya hawatakabiliwa na mashtaka ya mauaji tena na badala yake watakuwa mashahidi wa serikali katika kesi hiyo ya mauaji ambapo washukiwa wakuu bado wanazuiliwa. Wawili hao walikamatwa mnamo Agosti 11, 2024 kufuatia […]

FRANCE WAIBUKA WASHINDI

Kolo Muani na Ousmane Dembele walifungia Ufaransa bao moja kila mmoja wao na kuisaidia timu hiyo kuibuka na ushindi wa nyumbani kwa kuwalaza Ubelgiji 2-0 katika UEFA Nations League Jumatatu. Haikuwa timu ya Ufaransa yenye nguvu kamili iliyoingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huo mjini Lyon, huku nahodha Kylian Mbappe akiacha nje ikiwa ni moja […]

AMONDE ANA IMANI NA KIKOSI CHAKE

Kocha mkuu wa wachezaji saba wa KCB RFC Andrew Amonde anasema hamu yao ya kushinda mkondo wa tano wa mzunguko wa kitaifa wa saba saba huenda ikawagharimu taji hilo mjini Mombasa wikendi walipolazwa 12-15 na Kenya Harlequin katika fainali. Amonde anasema dakika chache za mvutano kwenye fainali ziliwagharimu mchezo hata anapotarajia kufanya marekebisho katika mkondo […]

CHAGUO LANGU MBAPPE

Mwanasoka nguli duniani, Cristiano Ronaldo amezua gumzo mitandaoni kwa mara ya kwanza baada ya kukiri chaguo lake la mchezaji bora kati ya Karim Benzema na Kylian Mbappe. Ronaldo bila shaka alikuwa na furaha ya kucheza pamoja na Benzema kwa miaka kadhaa wakati alipokuwa Real Madrid lakini Mbappe akiwa amewasili Bernabeu hivi majuzi, mashabiki walikuwa na […]

BENEAH ATAKA KUWEPO NA UTARATIBU

Mwanasoka wa zamani AbdulAziz Beneah ametoa onyo kwa wazazi, akiwataka kuwa waangalifu wanapowasajili watoto wao katika akademi za soka. Beneah aliibua wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa vyuo vya soka visivyo na maadili, ambavyo kulingana naye vinaweza kuathiri vibaya maisha ya watoto na matarajio ya baadaye katika mchezo huo. Beneah, ambaye pia ni kocha mkuu wa Makadara […]

NITALETA MABADILIKO

Mhandisi Richard Ngichabe Binga, mwenyekiti mpya aliyechaguliwa wa Shirikisho la Karate Kenya (KKF), ameahidi kuendeleza utamaduni wa uwazi na ukuzaji vipaji endelevu ndani ya shirika hilo. Binga alikiri haja ya mageuzi ili kuhakikisha uwazi katika usimamizi wa rasilimali na michakato ya maamuzi ya shirikisho. Binga, ambaye pia ni mwenyekiti wa klabu ya karate ya Hospitali […]

SERIKALI ITAANZISHA MIRADI YENYE THAMANI YA BILIONI 300 KASKAZINI NA KASKAZINI MASHARIKI MWA KENYA – GACHAGUA

Naibu Rais Rigathi Gachagua amethibitisha kuwa serikali imetanguliza maendeleo ya kasi ya Kaskazini na Kaskazini-Mashariki mwa Kenya kupitia miradi iliyolengwa ya mabilioni ya pesa inayotekelezwa pamoja na washirika. Kulingana na Gachagua miradi yenye thamani ya bilioni 300 chini ya Mpango wa Maendeleo ya Kaskazini na Kaskazini Mashariki (NEDI) inakusudiwa kuchochea mageuzi ya kijamii na kiuchumi […]