TUNA IMANI KUPATA USHINDI

Timu za mpira wa vikapu za Kenya kwa wachezaji wenye umri Chini ya miaka 23 mchezo wa 3×3 zimejawa na imani na ari huku zikijiandaa kwa Kombe lijalo la Dunia la FIBA 3×3 kwa U23 huko Ulaanbaatar, Mongolia. Timu za wanaume na wanawake, zinazojumuisha wachezaji wanane, makocha wawili, daktari wa timu, na mtaalamu wa fiziotherapi, […]

KENYA KUA WENYEJI KWA MASHINDANO YA DARTS

Kenya inajiandaa kuwa mwenyeji wa mashindano ya Afrika ya Darts Continental Tour ambayo pia yatatumika kama Mashindano ya Kufuzu kwa michuano ya Dunia ya Vishale Afrika kuanzia Septemba 27 hadi 29 jijini Nairobi. Mwenyekiti wa Kundi la Vishale la Buffalos Jeff Mureithi anasema michuano hiyo inaelekea kuvutia zaidi ya wachezaji 250 kote barani. Mshindi atajinyakulia […]

SINA HARAKA KUINGIA MARATHON

Bingwa wa Olimpiki mara mbili Beatrice Chebet anasema hana haraka ya kuhamia mbio za marathon lakini badala yake atatumia mbinu za taratibu kuhamia mbio za barabarani. Mshikilizi huyo wa rekodi ya dunia ya mbio za mita 10,000 ana nia ya kufuata nyayo za bingwa wa Boston Marathon Hellen Obiri na mshindi wa London Marathon 2023 […]

BULLETS NA ULINZI WAIMARISHA MAZOEZI

Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka nchini kwa akina dada Kenya Police Bullets na wenzao Ulinzi Starlets ambao ni mabingwa wa taji la FKF Women’s Cup wameimarisha mazoezi yao kuelekea mechi ya FKF Super cup mnamo Septemba tarehe 28. Maafande Kenya Police walishinda ligi kuu msimu jana kwa alama 49, huku Vihiga Queens na Ulinzi […]

NYOTA YA STARS YAREJEA

Mabao mawili kutoka kwake John Avire na Duke Abuya Jumanne uliipa Harambee Stars ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji Namibia katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2025 kwenye Uwanja wa Orlando jijini Johannesburg, Afrika Kusini. . Ushindi huo uliifanya Kenya kurejea kwenye mstari wa kampeni yake ya kufuzu kufuatia sare […]

WAHUDUMU WA JUAKALI WAHUSISHWA KWENYE MRADI WA NYUMBA ZA BEI NAFUU KWALE

Wahudumu wa sekta ya juakali katika kaunti ya Kwale wanatazamia kuimarisha biashara zao iwapo serikali kupitia idara ya nyumba na mipangilio ya miji itashirikiana nao katika utekelezaji wa mradi wa nyumba za bei nafuu. Kulingana na mkurugenzi wa mradi huo eneo la pwani John Karanja wahudumu wa juakali watapewa kandarasi ya kusambaza vifaa vya ujenzi […]

SENETA MANDAGO AREJEA MAHAKAMANI HUKU KESI YA KASHFA YA BILIONI MOJA IKIENDELEA

Seneta wa Uasin Gishu Jackson Mandago anatazamiwa kuendelea kusikilizwa leo, Jumatano 11, katika Mahakama ya Hakimu Mkuu ya Nakuru kujibu mashtaka ya ufisadi na ubadhirifu wa Ksh.1.1 bilioni zilizonuiwa kufadhili programu za ufadhili wa masomo kwa wanafunzi nchini Finland. Mandago na washtakiwa wenza pia watakabiliwa na mashtaka ya kula njama ya kutenda uhalifu wa kiuchumi, […]

SENETA CHIMERA RAPHAEL APENDEKEZA FEDHA ZA BASARI KUWEKWA CHINI YA UANGALIZI WA SERIKALI KUU

Seneta mteule Chimera Raphael Mwinzago anapendekeza usimamizi wa fedha za basari kuondolewa kwa wanasiasa na kuwekwa chinina uangalizi wa serikali ya kitaifa il k,uhakikisha elimu bila malipo kwa wote. Kwa mujibu wa Chimera kiasi cha pesa kilicho mikononi mwa wanasiasa kama basari iwapo kitatumika ipasavyo kinaweza kusaidia katika juhudi za kuziba mianya ya elimu shuleni […]

WAFANYIKAZI WA ANGANI WAGOMA WAKIPINGA MPANGO WA ADANI

Usafiri wa angani umetatizika baada ya wafanyikazi wa uwanja wa ndege wa JKIA kuanza rasmi mgomo wao. Kwa sasa hakuna ndege zinazopaa wala kutua katika uwanja wa JKIA. Wafanyikazi hao wamegoma kufuatia hatua ya serikali ya kutaka kukondisha uwanja wa kimataifa wa JKIA kwa kampuni ya india Adani Holdings. Imetayarishwa na Janice Marete

UPANZI WA MICHE KUREJESHA HADHI YA MSITU MT. ELGON

Serikali inapania kurejesha hadhi ya msitu wa Mlima Elgon ulioko kwenye kaunti ya Bungoma na Trans Nzoia kwa kupanda miche milioni 10 katika kipindi cha miaka 5 ijayo. Akizungumza na wanahabari, naibu mkurugenzi wa idara ya misitu Charity Munyasia amesema miche hiyo itapandwa kwenye ekari 7 za ardhi ya msitu huo. Aidha, amesema kwamba mradi […]