WATU WANNE WAFARIKI BAADA YA BOMBA LA MAJI TAKA KUPOROMOKA ENEO LA SHAURI MOYO JIJINI NAIROBI

Watu wanne wamefariki baada ya bomba la maji taka lililochimbwa kuporomoka katika mtaa wa Shauri Moyo jijini Nairobi. Msemaji wa Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS) Dkt Resila Atieno Onyango amesema kuwa operesheni ingali inaendelea katika eneo la tukio. Ameongeza kuwa watu watatu wameokolewa na wamehudumiwa. Kulingana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya, watu […]

WAKAAZI WA TRANSNZOIA WAMTAKA RUTO ATIMIZE AHADI ZAKE KWAO

Wakaazi wa kaunti ya Transnzoia wamemtaka rais William Ruto kutimiza ahadi alizotoa kwao wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2022. Kwa mujibu wa wakaazi hao rais Ruto aliahidi kuwapa shilingi milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa soko la Masinde Muliro Complex lililoko mjini Kitale na vile vile kuanzisha ujenzi wa nyumba za bei […]

WANAFUNZI SITA WAFARIKI KWENYE AJALI YA BARABARA YA KITUI – KIBWEZI

Watoto sita wa shule wamefariki katika ajali ya barabarani katika kituo cha biashara cha Wiitu kwenye barabara ya Kitui-Kibwezi. Akithibitisha kisa hicho cha Naibu Kamishna wa Ikitha Vincent Loctary Lomachary, amesema walioathiriwa ni pamoja na watoto watatu wa shule ya msingi na watatu wa shule ya upili. Kulingana na naibu kamishna wa kaunti, wanafunzi hao […]

RUTO AONYA WACHAFUZI WA NAIROBI RIVER

Rais William Ruto ametangaza onyo kali dhidi ya kampuni na watu binafsi ambao wamekuwa wakitupa taka ndani Nairobi River, akisema watawajibishwa kisheria. Akizungumza mtaani Korogocho jijini Nairobi wakati wa uzinduzi wa usafishaji wa mto huo, Rais amewaonya watakaokiuka agizo hilo kuwa tayari kuwajibikia mienendo yao. Aidha, ameahidi kwamba nafasi 200000 za ajira zitabuniwa chini ya […]

MASOMO YATATIZIKA CHUONI MOI KUSU IKIJIUNGA NA UASU

Shughuli za masomo katika chuo kikuu cha Moi zimesambaratika hata zaidi baada ya muungano wa wafanyakazi wa vyuo vikuu KUSU eneo hilo kujiunga na wenzao wa UASU kwenye mgomo ambao umelemaza masomo kwa wiki ya tatu sasa. Wanachama wa UASU na KUSU wameandamana jijini Eldoret wakishinikiza kulipwa mishahara yao na kuwasilisha matozo ya fedha za […]

UTULIVU WAREJEA MARIKITI, VIUNGA VYAKE

Utulivu umerejea kwenye maeneo yaliyo karibu na soko la wakulima katika barabara ya Haile Selassie jijini Nairobi ambapo kimeshuhudiwa mapema leo kufuatia makabiliano baina ya maafisa wa polisi na wafanyabiashara ambao wanapinga kuhamishwa kutoka soko hilo. Kwa zaidi ya kipindi cha saa 5 polisi na askari wa kaunti wamekuwa wakiwakabili wafanyabiashara hao kwa vitoza machozi […]

MMELEMAZA AFYA, AYACKO AISUTA HAZINA KUU

Gavana wa Migori Ochillo Ayacko ameikashifu hazina ya kitaifa kwa madai ya kuhujumu utekelezaji wa mpango wa afya kwa wote kutokana na ukosefu wa fedha kwenye serikali za kaunti. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa vituo vya afya kwenye kaunti hiyo, Ayacko amefadhaishwa na uchelewashaji wa mara kwa mara wa utoaji wa mgao wa kaunti na […]

RUTO; WAFISADI WATAONA CHA MTEMA KUNI

Wafisadi wametakiwa kuacha mara moja kujinufaisha na mali ya umma kwani kulingana na Rais william Ruto watakabiliwa kwa mujibu wa sheria. Ruto aidha ameahidi kuhakikisha kuna uwazi serikalini akisema kuwa yeye binafsi yuko tayari kuwajibishwa,kujukumishwa na kukosolewa. Katika hotuba yake wakati wa kuzindua mpango wa kimkakati wa kitaifa ushirikiano na utawala bora rais. Ruto ametangaza […]

MWANAMKE, WA MIAKA 32, AUAWA KATIKA SOKO LA DARAJA MBILI HUKO KISII

Polisi mjini Kisii wanachunguza kisa ambapo mwanamke mwenye umri wa miaka 32 amepatikana akiwa amefariki katika kijiji cha Mwamogesa Moraa katika Kaunti Ndogo ya Kitutu ya Kati. Kulingana na polisi, marehemu kwa jina la Molly Achieng’, ambaye alikuwa akiishi katika kijiji jirani, amepatikana akiwa kwenye dimbwi la damu huku akiwa na majeraha kichwani na usoni. […]

WAFANYABIASHARA KATIKA SOKO LA MARIKITI WAANDAMANA KUPINGA KUFUKUZWA KATIKA SOKO HILO

Shughuli za biashana na usafiri zimetatizika katika barabara ya jogoo road na Haile Selasie Avenue baada ya wafanyibiashara wanaofanya biashara katika soko la Wakulima, maarufu Marikiti, kuandamana mapema leo wakiapa kusitisha shughuli zao hadi pale serikali ya kaunti itakapoondoa notisi ya kuwafurusha katika soko hilo. Kulingana na wafanyabiashara hao, maafisa wa Baraza la Kaunti walifika […]