WAKAZI SOUTH C WAANDAMANA KUHUSU USALAMA WA MAJENGO
Wakazi wa South C wamefanya maandamano ya amani wakilalamikia kuporomoka kwa jengo la makazi mapema mwaka huu katika barabara ya Muhoho huku wakitaka hatua madhubuti zichukuliwe
Maandamano hayo yaliyoishia katika bustani ya Uhuru yaliwaleta pamoja wakazi viongozi wa eneo na wanaharakati waliodai uwajibikaji pamoja na utekelezaji mkali wa sheria za ujenzi
Wakazi wameonya kuwa jengo lingine katika eneo hilo liko hatarini kuporomoka wakitoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka na kufanya uchunguzi wa kina ili kuwachukulia hatua waliohusika na pia kuimarisha ufuatiliaji ili kuepuka majanga kama hayo siku zijazo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































