#Local News

MWANAMME ADAIWA KUMWUA MWANAWE KWA UPANGA

Polisi katika kaunti ya Kakamega wanaendeleza uchunguzi katika tukio ambapo mwanamme mmoja katika Kijiji cha Emabusi eneo bunge la Ikolomani, ameripotiwa kumuua mwanawe kwa kumkatakata na kuwajeruhi wengine vibaya.

Mwanamme huyo aliyeshambuliwa na wananchi wakati wa tukio hilo, anatibiwa hospitalini chini ya ulinzi mkali, huku walioshuhudia tukio hilo wkaisema alichukua hatua hiyo kutokana na mzozo wa kinyumbani na mkewe.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *