MATIANG’I AKOSOA G2G
Mwaniaji wa urais kwa tiketi ya chama cha Jubilee Fred Matiang’i, ameikosoa serikali kutokana na kupanda kwa bei za mafuta, akihusisha ongezeko hilo na mpango wa uagizaji wa mafuta wa G2G anaosema haueleweki.
Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Matiang’i ameitaka serikali kuweka wazi maelezo ya mpango huo, akitilia shaka hatua ya serikali kutolihusisha shirika la kitaifa la mafuta, NOC kwenye mpango huo.
Kulingana naye, G2G imetumika kufuja fedha.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































