#uncategorized

MATHARE UNITED WOMEN WAPANDA DARAJA KURUDI LIGI KUU

Kikosi cha Mathare United Women kimehakikisha kupanda daraja kuelekea ligi kuu ya wanawake nchini baada ya kampeni nzuri katika Ligi ya Taifa ya Daraja la Pili

Timu hiyo ilithibitisha mafanikio yake kwa ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Gitothua mwishoni mwa wiki ushindi ulioweka wazi ubabe wao msimu huu na kurejea kwao katika kiwango cha juu baada ya miaka minne

Kocha mkuu Anne Aluoch amesema mafanikio hayo yametokana na maandalizi mazuri msaada wa wadhamini pamoja na uzoefu wa klabu hiyo katika ligi ya NSL akisisitiza kuwa mipango ya mapema ilichangia pakubwa katika mafanikio yao ya kupanda daraja.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *