#Football #Sports

CHECHE AITAKA JUNIOR STARLETS KUDUMISHA NIDHAMU KABLA YA MECHI YA UGANDA

Kocha mkuu wa Junior Starlets Mildred Cheche amewataka wachezaji wake kubaki na nidhamu na kutojisahau huku wakijiandaa kwa mchezo wa pili wa mchujo wa Kombe la Dunia la wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba

Starlets wanatarajiwa kukutana na upinzani mkali kutoka Uganda katika hatua hii baada ya kuibwaga Namibia kwa jumla ya mabao saba kwa moja katika michezo miwili ya awali

Kenya walishinda ugenini Windhoek kwa mabao mawili kwa moja kabla ya kukamilisha kazi kwa ushindi wa mabao matano kwa bila nyumbani katika uwanja wa Ulinzi Sports Complex huku Cheche akisisitiza utulivu umakini na nidhamu katika mechi zijazo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

CHECHE AITAKA JUNIOR STARLETS KUDUMISHA NIDHAMU KABLA YA MECHI YA UGANDA

WALIMU WA JSS WATANGAZA MGOMO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *