LEICESTER CITY WASHUSHWA LEAGUE ONE
Klabu ya Leicester City imeshushwa daraja kutoka Championship hadi League One, miaka 10 baada ya kushinda ligi kuu ya Uingereza, EPL, miaka 5 tangu kushinda taji la FA, na msimu mmoja tu baada ya kushushwa daraja kutoka EPL.
Hatma yao ilitiwa muhuri jana usiku baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Hull City, na kuwaacha mabingwa hao wa EPL mwaka 2016 wakiwa na pointi 42 katika nafasi ya 23.
Masaibu yao yalianza baada ya kupokonywa pointi 6 walipopatikana na hatia ya kukiuka sheria za matumizi ya fedha, wafuasi wa klabu hiyo wakishinikiza kuvunjwa kwa bodi ya klabu hiyo.
Kwa sasa hawana budi ila kujiandaa kwa maisha ya daraja la 3 la soka nchini Uingereza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































