HARAMBEE STARLETS WAPANDA NGAZI YA FIFA
Timu ya taifa ya soka ya wanawake, Harambee Starlets juu kwa nafasi 5 na kufikia nafasi ya 128 duniani katika jedwali la FIFA kutokana na mchezo mzuri walioonyesha katika mashindano ya FIFA Series yaoliyokamilika wiki jana jijini Nairobi.
Kupanda huko kumetokana na ushindi dhidi ya India waliokuwa wameorodheshwa katika nafasi ya 69, na kufungwa mabao 2 pekee na Australia waliokuwa wameorodheshwa katika nafasi ya 15 duniani.
Mataifa ya bara Afrika yaliyo katika nafasi za juu kwenye jedwali hilo ni Nigeria walio katika nafasi ya 36, Afrika Kusini katika nafasi ya 58 na Zambia katika nafasi ya 64.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































