CAVB: KCB KUPEPERUSHA BENDERA YA KENYA FAINALI
Klabu ya voliboli KCB itaiwakilisha Kenya katika fainali za mashindano ya ubingwa wa klabu za voliboli za wanawake barani Afrika jijini Cairo, Misri, kufuatia ushindi dhidi ya wenzao kutoka nchini, Kenya Pipeline seti 3-1 katika semi fainali za mashindano hayo hapo jana.
Wanabenki hao walikabiliwa na ushindani mkali, wakikabana seti 1-1 kabla ya KCB kushinda seti za 3 na 4 kukata tiketi ya fainali.
Timu ya DCI iliyobanduliwa na Kenya Pipeline katika awamu ya robo fainali, itashiriki kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya 5 baada ya kuilaza MKE ya Cameroon seti 3-0.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































