#Local News

BAADHI YA MCA NAIROBI WAMWOMBA RUTO AINGILIE KATI KUOKOA JIJI

Sehemu ya wawakilishi wadi wa jiji la Nairobi wamemwomba Rais William Ruto kuingilia kati na kusaidia kurekebisha hali ya jiji wakidai uongozi wa sasa umeshindwa kutekeleza majukumu yake

Wakiongozwa na Mwakilishi wadi wa  Nairobi South Waithera Chege viongozi hao wamemtuhumu gavana Johnson Sakaja kwa ubaguzi wa baadhi ya maeneo na kushindwa kuboresha huduma kwa wananchi

Hata hivyo wanakumbusha kuwa Rais Ruto na Sakaja walitia saini makubaliano ya ushirikiano yenye thamani ya shilingi bilioni themanini mwezi Februari wakisema sasa ni wakati wa utekelezaji kuonekana ili kuinua hali ya jiji.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *