11 KUSHTAKIWA KUHUSIANA NA MAANDAMANO
Waandamanaji 11 waliokamatwa jana na polisi jijini Nairobi wakati wa maandamano ya kupinga bei mpya za juu za mafuta wanatarajiwa kufukishwa mahakamani hii leo.
11 hao walikamatwa na maafisa wa DCI waliokuwa wamevalia mavazi ya raia, kamanda wa polisi eneo la Nairobi Issa Mohamud akithibitisha kukamatwa huko.
Miongoni mwa waliokamatwa ni mwanaharakati Julius Kamau.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































