KAMWOROR KUREJEA LONDON MARATHON AKITAFUTA REKODI MPYA
Mshindi mara mbili wa New York City Marathon Geoffrey Kamworor anatarajiwa kurejea kwenye mbio za London Marathon Jumapili hii akiwa na lengo la kuboresha na kuvuka kiwango chake bora alichowahi kukimbia
Katika mashindano ya mwaka 2023 Kamworor alikimbia muda wake bora zaidi wa saa mbili dakika nne na sekunde ishirini na tatu katika mbio za kilomita arobaini na mbili ambapo alishika nafasi ya tatu nyuma ya marehemu Kelvin Kiptum na Tamirat Tola wa Ethiopia
Kamworor amesema anarejea London akiwa na ari mpya na azma ya kuboresha muda wake huku akilenga kuonesha ushindani mkali katika mbio hizo za kimataifa zinazotarajiwa kuvutia wanariadha bora duniani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































