#Local News

SERIKALI YATOA FEDHA ZA UFADHILI KWA MUHULA WA PILI

Serikali imetoa shilingi bilioni ishirini na tatu nukta nne za ufadhili kwa shule za umma kabla ya kufunguliwa kwa muhula wa pili Jumatatu ili kuhakikisha shughuli za masomo zinaendelea bila usumbufu

Katibu Mkuu wa Elimu ya Msingi Julius Bitok amesema fedha hizo zitaingia katika akaunti za shule kufikia Ijumaa ili kuwapa wasimamizi muda wa kujiandaa ipasavyo kwa ufunguzi wa shule

Ameongeza kuwa serikali pia inaweka kipaumbele katika usambazaji wa vifaa vya kujifunzia ikiwemo vitabu vya darasa la kumi kama sehemu ya utekelezaji wa mfumo mpya wa elimu unaolenga kuimarisha ujuzi wa wanafunzi.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *