GUARDIOLA ASEMA HANA PRESHA MSIMU HUU
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana wasiwasi wowote msimu huu akieleza kuwa hali ni tofauti kabisa na ilivyokuwa msimu uliopita
Amesema msimu uliopita ulikuwa na presha kubwa kwani alihofia kushindwa kuipeleka timu katika mashindano ya Ulaya lakini sasa mambo yako shwari zaidi
Guardiola ameongeza kuwa kwa sasa timu iko tulivu na yenye kujiamini zaidi hata kabla ya ushindi wao dhidi ya Arsenal hali inayowapa matumaini makubwa katika mechi zijazo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































