IEBC YASISITIZA MWISHO WA USAJILI WA WAPIGA KURA NI APRILI 28
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC imesisitiza kuwa zoezi la usajili wa wapiga kura halitaongezewa muda na litakamilika Aprili ishirini na nane mwaka elfu mbili ishirini na sita.
Akizungumza katika eneo la Iten Kaunti ya Elgeyo Marakwet, Mwenyekiti wa tume hiyo Erastus Ethekon ameonya dhidi ya kuingiza siasa katika mchakato huo akisisitiza kuwa unapaswa kubaki huru na wa haki kwa wote.
Amehakikisha kuwa tume imejizatiti kuwafikia wananchi wote wanaostahili kujiandikisha huku akiwahimiza kujitokeza kwa wingi kabla ya muda uliopangwa kukamilika.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































