#Local News

WIZARA YA AFYA YAONYA KUHUSU MLIPUKO WA MAGONJWA KISA TAKATAKA

Wizara ya afya imesema kuwa wakenya wengi wako katika hatari ya maambukizi ya magonjwa kutokana na ongezeko la taka zinazotupwa ovyo ovyo.

Katibu mkuu katika wizara ya afya Mary Muthoni amesema kuwa kwa sasa wakenya hasa walio katika maeneo ya miji ndio walio katika hatari kubwa ya mlipuko wa magonjwa hayo.

Aidha takwimu zimeonyesha kuwa kenya huzalisha takriban tani elfu 22 kwa siku huku asilimia kumi zikiwa ndizo zinazosimamiwa ipasavyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *