#Football #Sports

LIVERPOOL KARIBU KUMALIZANA NA KONATE KUHUSU MKATABA MPYA

Klabu ya Liverpool iko karibu kufikia makubaliano kamili na beki Ibrahima Konate kuhusu kusaini mkataba mpya baada ya mazungumzo kuendelea vizuri

Mazungumzo hayo yamepata msukumo mpya kufuatia kusimama kwa mawasiliano yaliyokuwa yakihusisha Real Madrid mwezi Novemba hatua iliyofungua nafasi kwa Liverpool kuendelea na mazungumzo

Ingawa makubaliano hayajakamilika rasmi bado klabu hiyo ina imani kubwa kuwa yatafikiwa hivi karibuni huku ikilenga kumhifadhi mchezaji huyo muhimu katika kikosi chake.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *