#Local News

ATWOLI AWASUTA WANAOIBUA MADAI KUHUSU KIFO CHA RAILA

Katibu mkuu wa COTU Francis Atwoli amewasuta baadhi ya viongozi wanaoibua madai kuhusiana na kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga.

Atwoli amesema kuwa Raila hakuwa mtu wa kawaida na alikuwa na heshima zake kisiasa na hivyo kuibua madai yasiyo na msingi kuhusiana na kifo chake ni kutofanyia haki familia yake.

Aidha, amewaomba wale wanaosema kuwa kifo chake hakikua cha kawaida kutoa ushahidi kuhusiana na swala hilo kwa umma na vyombo vya kisheria huku akiomba nafasi kwa familia ya Odinga iweze kupona kutokana na kifo cha hayati Odinga.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *