#Football #Sports

RACHIER AHOJI VIWANGO VYA MAREFA KABLA YA MASHEMEJI DERBY

Mwenyekiti wa Gor Mahia Ambrose Rachier ameibua wasiwasi kuhusu viwango vya uamuzi wa marefa katika ligi kuu ya soka nchini siku chache kabla ya dabi ya Mashemeji inayotarajiwa kufanyika Jumapili Aprili ishirini na sita

Rachier amehoji uthabiti wa maamuzi ya waamuzi akionya kuwa makosa katika hatua hii ya msimu yanaweza kuathiri pakubwa mbio za ubingwa na msimamo wa ligi

Kauli yake inafuatia tukio tata katika mechi kati ya Gor Mahia na Bandari ambapo penalti iliyokuwa imetolewa ilifutwa baadaye hali iliyozua mjadala mkubwa huku akitaka uwajibikaji zaidi na matumizi ya sheria kwa usawa katika mechi zote.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *