#Sports

MATINEJA WA KENYA WAZIDI KUNG’AA ANGOLA

Idadi ya medali za taifa la Kenya katika michezo ya wanaspoti wa kati ya umri wa miaka 14-17 ya 2025 Africa Youth Games inayoendelea nchini Angola imepanda hadi 14, baada ya kikosi cha mchezo wa judo na fencing kujizolea medali 3 zaidi za shaba.

Rael Kulova na harun Amin walishinda nishani 2 za shaba huku Kinoti Kiara akishinda shaba katika mchezo wa fencing, Kenya sasa ikiwa na dhahabu 4, fedha 3 na shaba 7.

Kulova anayeorodheshwa wa 93 katika kitengo cha matineja na 233 kwa jumla ulimwenguni, alimpiku mwenzake wa Nigeria katika kiwango cha uzani usiozidi kilo 44.

Ushindi huo unaongeza nakshi kwenye mwaka huu kwa mtindo wa aina yake, baada ya kuibuka mshindi kwenye mapigano kadhaa ikwemo nishani ya dhahabu katika mashindano ya Casablanca cadet African Cup mapema mwaka huu nchini Morocco, na shaba katika mashindano ya Pretoria Cadet African Cup na Pretoria Junior African Cup nchini Afrika Kusini.

Tineja huyo mwenye umri wa miaka 16 amesema anaangazia kuiwakilisha Kenya katika mashindano ya 2026 Youth Olympics jijini Dakar nchini Senegal.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MATINEJA WA KENYA WAZIDI KUNG’AA ANGOLA

KPL YAPAMBA MOTO

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *