HALI YA GRADE 10
Asilimia 92 ya wanafunzi waliofanya mtihani wa gredi ya 9 mwaka jana wamejiunga na gredi ya 10 katika shule za sekondari ya juu, na juhudi zimeimarishwa ili kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wameripoti shuleni.
Haya ni kulingana na naibu rais Kithure Kindiki, akikariri agizo la Rais William Ruto la kuwataka wanafunzi kuripoti shuleni licha ya ukosefu wa karo.
Naye Waziri wa elimu Julius Ogamba, amewaonya walimu wakuu dhidi ya kukiuka agizo la Rais Ruto.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 









































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































