SERIKALI YAANZISHA UJENZI WA THIKA STADIUM
Serikali imeanzisha ujenzi wa uwanja wa Thika Stadium wenye uwezo wa kuwabeba mashabiki 10,000, ambao huenda ukatumiwa kwa mazoezi wakati wa dimba la mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao, AFCON 2027.
Ujenzi huo umekadiriwa kugharimu shilingi milioni 850, serikali ikisema utakamilika kufikia mwishoni mwa mwaka huu.
Thika Stadium inatarajiwa kuchukua mahala pa Thika Municipal Stadium ambao umekuwa katika hali duni kwa miaka.
Waziri wa michezo Salim Mvurya, amewahakikishia wafanyabiashara walio karibu na uwanja huo mpya kwamba ujenzi huo hautasambaratisha biashara zao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































