DOZI YA KWANZA YA PREP KUKABILI UKIWMI YAWASILI
Juhudi za serikali kukabili maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI zimepigwa jeki kufuatia kuwasili kwa shehena ya kwanza ya dozi 21,000 za dawa ya kinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo yaani PREP inayodungwa, dozi nyingine 12,000 zikitarajiwa kuwasili nchini mwezi Aprili.
Shehena hiyo imewasilishwa kupitia ushirikiano kati ya serikali na shirika la Global Fund, dozi 25,000 kutoka kwa serikali ya Marekani pia zikitarajiwa kuimarisha awamu ya kwanza ya mpango huo unaolenga kupanua upatikanaji wa teknolojia bunifu ya kuzuia maambukizi ya UKIMWI.
Wizara ya afya itatekeleza mpango huo kwa awamu kuanzia mwezi ujao kwenye kaunti 15 zilizoorodheshwa kuwa na mamabukizi ya juu kabla ya kuutekeleza katika kaunti nyingine.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































