RUTO ATETEA BEI ZA JUU ZA MAFUTA
Rais William Ruto ametetea bei ya juu ya mafuta nchini ikilinaginishwa na mataifa mengine katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, akisema sababu ni kwamba Kenya inakuwa kiuchumi zaidi ya mataifa hayo.
Akizungumza jijini Nairobi kabla ya kuelekea Italia kwa ziara ya siku 3, Ruto amesema kiwango cha miundomsingi ya barabara zilizojengwa nchini kinazidi kile cha mataifa hayo kwa pamoja.
Kulingana naye, ushuru wa mafuta unahitajika pakubwa kuimarisha barabara.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































