#Local News

LINDA MWANANCHI YATOA MASHARTI KWA LINDA GROUND

Viongozi wa ODM wanaoegemea mrengo wa Linda Mwananchi unaoongozwa na katibu mkuu Edwin Sifuna wamesema kwamba wako tayari kushiriki mazungumzo na mrengo wa kinara Oburu Oginga, iwapo mrengo huo utakubali kuachilia nyadhifa za uongozi na kuruhusu uchaguzi mpya.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara jijini Nakuru, Linda Mwananchi pia wamewataka wenzao wa Linda Ground kusitisha kampeni za kumpigia debe Rais William Ruto kuchaguliwa kwa muhula wa pili iwapo wanataka mazungumzo.

Miongoni mwa viongozi hao ni gavana James Orengo, seneta Godfrey Osotsi na wabunge Caroli Omondi na Babu Owino.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

LINDA MWANANCHI YATOA MASHARTI KWA LINDA GROUND

MATIANG’I AKOSOA G2G

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *