WATU KADHAA WAKAMATWA KATIKA MAANDAMANO YA MAFUTA NAIROBI
Takriban watu kumi na mmoja wamekamatwa baada ya kujaribu kuandamana jijini Nairobi kupinga kupanda kwa bei ya mafuta
Polisi wa kutuliza ghasia waliwatawanya waandamanaji hao walipokuwa wakijaribu kuelekea katikati ya jiji kutoka eneo la Archives na kuwapeleka katika kituo cha polisi cha Central
Kamanda wa polisi wa Nairobi Issa Mohamud amesema maafisa walikuwa wakishirikiana na kundi hilo kudumisha utulivu akiongeza kuwa hali ya jiji ilikuwa tulivu kwa sehemu kubwa ya asubuhi
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































