#Local News

WALIMU WA JSS WATANGAZA MGOMO

Huku wanafunzi wakijiandaa kurejea shuleni kwa muhula wa pili wiki ijayo, huenda shughuli za masomo katika shule za sekondari msingi, JSS zikatasambaratika kutokana na mgomo wa walimu wa shule hizo ulioratibiwa kuanza Jumatatu.

Lengo la mgomo huo ni kuishinikiza serikali kuwapa ajira ya kudumu, mbali na bima ya afya wakisema wamekuwa wakinyimwa huduma za matibabu chini ya SHA katika baadhi ya hospitali nchini.

Kupitia muungano wa KUPPET, walimu hao wamedai kugharamikia matibabu licha ya serikali kushikilia kuwa SHA inafanya kazi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *