IEBC YASISITIZA MUDA WA USAJILI HAUTAONGEZWA
Huku zoezi linaloendelea la usajili wa wapiga kura wapya likikaribia kutamatika, tume huru ya uchaguzi na mipaka imepuzilia mbali uwezekano wa kuongeza muda wa usajili, ikisisitiza kuwa zoezi hilo litakamilika Jumapili hii jinsi ilivyopangwa.
Kulingana na tume hiyo, imetoa fursa kwa kila mkenya katika kila eneo kujisajili, ikiwataka ambao hawajasajiliwa kutumia muda uliobaki wa takribani siku 6.
Wakati uo huo, spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula, ameiagiza kamati ya masuala ya kisheria kuchunguza madai ya mbunge wa Embakasi West Mark Mwenje kwamba IEBC inawahamishia baadhi ya wapiga kura wa Nairobi katika kaunti ya Garissa kinyume na sheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































