MURKOMEN: KUNA MAELFU YA WAHUNI NCHINI
Imebainika kwamba kuna magenge 100 yenye maelfu ya wanachama ambayo yanaendelea kuvuruga mikutano ya kisiasa nchini, serikali ikidai magenge hayo yanafadhiliwa na baadhi ya wanasiasa.
Akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu usalama, Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, ameilaumu idara ya mahakama kutokana na ongezeko la uhuni, akisema idara hiyo imelegeza masharti.
Aidha, amesema washukiwa 14 kati ya 17 waliomshambulia seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi walitorokea nchi jirani na wanasakwa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































