#Local News

RUTO AHOJI UFANISI WA UMOJA WA MATAIFA

Rais William Ruto ameibua wasiwasi kuhusu ufanisi na uaminifu wa Umoja wa Mataifa akisema chombo hicho kinakabiliwa na changamoto katika kudhibiti mivutano ya kisiasa duniani

Akizungumza katika chuo kikuu cha LUISS nchini Italia Rais amesema mfumo wa kimataifa wa amani na usalama unaoongozwa na Umoja wa Mataifa unaonekana kudhoofika huku nguvu za mataifa makubwa zikichukua nafasi ya sheria

Kauli hiyo inajiri wakati dunia ikishuhudia ongezeko la migogoro na hali ya kutokuwa na utulivu ambapo Rais amesisitiza haja ya kuimarisha mifumo ya kimataifa ili kudumisha amani na usalama duniani.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *