IEBC: HATUTARUHUSU WANASIASA WANAOTUMIA WAHUNI KWENYE UCHAGUZI
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imewaonya wanasiasa wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi nchini dhidi kuwatumia vijana kuvuruga mikutano ya kisiasa.
Akizungumza kwenye mkutano na washikadau kaunti ya Turkana, Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema wanasiasa watakaopatikana wakijihusisha na kutumia wahuni hawataruhisiwa kuwania wadhifa wowote nchini.
Kauli hiyo inajiri huku kukiwa na shinikizo la kudhibiti wahuni nchini huku wakaazi wa Turkana wakiitaka tume hiyo kuimarisha juhudi za usajili wa wapiga kura.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































