#Local News

WINGU LA UFUSADI LATANDA BUNGENI

Idara ya bunge sasa inakabiliwa na wakati mgumu kujitakasa kutokana na madai ya ufisadi dhidi yake, tuhuma kwamba maseneta hupokea rushwa kutoka kwa magavana zikiingia katika bunge la kitaifa.

Wa hivi punde kuhusishwa na ufisadi ni mbunge wa Bumula Jack Wamboka, ambaye ametimuliwa kutoka wadhifa wa mwenyekiti wa kamati ya uwekezaji wa umma kutokana na madai ya kuitisha hongo kutoka mwenyekiti wa tume ya kitaifa ya uwiano na utangamanao, NCIC, Samuel Kobia.

Naibu spika wa bunge la kitaifa Gladys Shollei, amemwagiza kiongozi wa wachache kumteua mwenyekiti mpya atakayeshikilia wadhifa huo hadi uchunguzi dhidi ya Wamboka utakapokamilika.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *