SHA YAAHIDI BIMA BORA KWA WALIMU KUEPUSHA MGOMO
Huenda mgomo wa walimu wa shule za sekondari msingi JSS uliokuwa ukitishia kusambaratisha masomo kuanzia wiki ijayo, ukasitishwa, kufuatia hatua ya bima ya SHA kuahidi kushughulikia malalamishi ya walimu hao kuhusiana na huduma za matibabu chini ya bima hiyo.
Kwenye mkutano na viongozi wa miungano ya kutetea maslahi ya walimu, KNUT na KUPPET, SHA imesema walimu hawatatoa fedha za ziada maarufu kama copay kulipia matibabu chini ya bima hiyo, ikisema bima hiyo itapigwa msasa upya ili kukidhi mahitaji ya walimu.
Afisa mkuu mtendaji wa SHA, Dr. Mercy Mwangangi, amezionya hospitali dhidi ya kuwatoza walimu malipo ya copay.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































