MIANYA YA UFADHILI WA MASOMO
Maswali yameibuka kuhusu gharama ya kufadhili masomo katika shule za umma, ikibainika kuwa wanafunzi milioni 3.4 walikosa ufadhili katika kipindi cha kati ya mwaka 2020-2024 kufuatia hatua ya serikali kukosa kutuma mgao wa shilingi bilioni 117 kufanikisha masomo ya bila malipo.
Kulingana na ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali, serikali inaendelea kulemewa na mzigo wa kufadhili elimu ya bure katika shule za umma, idadi ya wanafunzi waliokosa ufadhili huo ikipanda kutoka 724,000 katika mwaka wa kifedha wa 2020-21 hadi milioni 1.1 mwaka 2023-24.
Huku serikali ikitangaza upungufu zaidi mwaka ujao, wabunge wametilia shaka masuala yanayopewa kipaumbele.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































