#Local News

MURKOMEN AWATETEA POLISI DHIDI YA UVAMIZI NYERI

Waziri wa usalama wa kitaifa Kipchumba Murkomen, ameitetea idara ya polisi kuhusiana na uvamizi wa kanisa moja kaunti ya Nyeri wakati wa ibada iliyokuwa ikihudhuriwa na aliyekuwa naibu Rais Rigathi Gachagua mapema mwaka huu.

Akiwa mbele ya bunge, Murkomen amesema uvamizi huo ulisababishwa na uhasama wa kisiasa miongoni mwa viongozi wa kisiasa wa eneo hilo, akiongeza kuwa asasi za kiusalama hazikufahamishwa kuhusu uwepo wa viongozi wa ngazi ya juu kwenye ibada hiyo.

Aidha, ametetea hatua ya maafisa wa polisi kuficha nyuso zao wakati wa operesheni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *