#Football #Sports

USIMAMIZI MBAYA WA MECHI WAKOSOLEWA KPL

Washikadau katika sekta ya kabumbu nchini wamelalamikia madai ya uendeshaji mbaya wa mechi za ligi kuu ya soka nchini, KPL, wakilitaka shirikisho la soka FKF kuwachukulia hatua marefa wanaokiuka sheria za kandanda.

Miongoni mwao ni mwenyekiti wa klabu ya Gor Mahia Ambrose Rachier, akisema mwenendo huo unaiharibia jina soka ya Kenya.

Rachier amehusisha usimamizi huo na matokeo duni yaliyoandikishwa na Gor Mahia katika mechi za mwisho za ligi walizocheza, akisema walinyimwa mikwaju miwili ya penalti katika mechi dhidi ya Tusker FC ambako walipoteza bao 1-0, na katika mechi dhidi ya Bandari iliyoishia sare ya kutofungana.

Akizungumza na wanahabari, Rachier ameibua hofu kwamba huenda ukiukaji wa sheria za soka unalenga kushawishi ubingwa wa taji la KPL msimu huu unaoelekea ukingoni.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *