#Football #Sports

GNABRY KUKOSA KOMBE LA DUNIA KUTOKANA NA JERAHA

Mshambulizi wa klabu ya Bayern Munchen na timu ya taifa ya Ujerumani, Serge Gnabry, amethibitisha kwamba hatashiriki mashindano ya kombe la dunia mwaka huu kutokana na jeraha la paja.

Tangazo lake linajiri baada ya Beyern siku ya Jumamosi kutangaza kwamba alikuwa ameratibiwa kukosa ilichotaja kwamba muda mrefu kutokana na jeraha hilo, vyombo vya habari nchini Ujerumani vikiripoti kuwa angekosa mashindano hayo.

Gnabry mwenye umri wa miaka 30, amesema hatakuwa uwanjani tena msimu huu, na kujiondoa katika mashindano ya kombe la dunia yatakayoandaliwa katika mataifa ya Marekani, Mexico na Canada kuanzia mwezi Juni.

Kupitia ujumbe aliochapisha kwenye mitandao ya kijamii, Gnabry amesema kwa sasa ataelekeza makini yake katika kuuguza jeraha hilo.

Mshambulizi huyo wa zamani wa Arsenal amekuwa nguzo kwenye kikosi cha mkufunzi Julian Nageslmann, akifunga mabao 26 katika mechi 59 kwa taifa.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *