KENYA YAWEKA JUHUDI ZA KUONGEZA UZALISHAJI WA NDANI WA BIDHAA ZA AFYA
Serikali kuu inalenga kuwa kitovu cha kikanda katika uzalishaji wa bidhaa za afya kwa kutumia motisha ya kifedha, marekebisho ya kisheria, uvumbuzi, na wafanyakazi wenye ujuzi.
Wakizungumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya afrika 2026 MEDEXPO, maofisa waandamizi nchini wamesema uzalishaji wa ndani wa bidhaa za afya kama vile dawa muhimu, vipimo, na chanjo utaiwezesha Kenya kuwa salama dhidi ya usumbufu unaoweza kujitokeza kwenye mnyororo wa usambazaji wa dunia, unaosababishwa na migogoro na mabadiliko ya tabianchi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Biashara Regina Akoth Ombam amesema serikali imeweka kipaumbele katika kuongeza uzalishaji wa teknolojia za afya na bidhaa muhimu za afya kwa ajili ya matumizi ya ndani na nje, kama inavyoelekezwa kwenye ajenda ya taifa ya mabadiliko ya viwanda.
Imetayarishwa na Maurine Amwayi
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































