#Business

PAOK YAONYA KUHUSU ONGEZEKO LA BEI YA MAFUTA NCHINI

Muungano wa Vituo vya Mafuta nchini (PAOK) umekosoa uamuzi wa serikali wa kupunguza ushuru wa ongezeko la thamani (VAT) kwa bidhaa za petroli, ukisema kuwa hatua hiyo haiwezi kutoa afueni kubwa kwa watumiaji.

Kulingana na muungano huo, manufaa yoyote ya muda mfupi yanaweza kuzidishwa na ukosefu wa ufanisi ndani ya mfumo wa uagizaji mafuta na bei.

Akizungumza wakati wa mahojiano kwenye kituo kimoja cha runinga Mwenyekiti wa PAOK, Martin Chomba ameonya kwamba upunguzaji wa ushuru unaweza hatimaye kusababisha bei ya juu ya mafuta ikiwa masuala ya kimfumo yatasalia bila kutatuliwa, akiongeza kuwa bila usimamizi bora wa ununuzi, usambazaji na udhibiti wa soko, kuingilia kati kwa serikali kunaweza kuwa na athari ndogo katika kuleta utulivu.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *