#Local News

SERIKALI YABINAFSISHA KENYA PIPELINE COMPANY

Hazina ya Taifa imebatilisha hadhi ya Kampuni ya Kenya Pipeline (KPC) kama shirika la serikali kupitia notisi ya gazeti rasmi, hatua inayothibitisha mabadiliko yake kuwa kampuni ya umma iliyoorodheshwa

KPC sasa imegeuka rasmi kuwa kampuni ya umma baada ya serikali kuuza asilimia sitini na tano ya hisa kupitia ofa ya awali ya hisa katika Soko la Hisa la Nairobi

Serikali sasa inamiliki asilimia thelathini na tano ya hisa huku ubinafsishaji huo ukilenga kukusanya takriban shilingi bilioni mia moja na sita nukta tatu kutoka kwa wawekezaji wa ndani na nje pamoja na kukuza ukuaji wa muda mrefu wa kampuni hiyo.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *