TUSKER YAONYESHA MABADILIKO CHINI YA KOCHA METTE
Kocha mkuu wa Tusker Julien Mette amesema wachezaji wake sasa wanaanza kuzoea falsafa yake ya kiufundi huku matokeo ya hivi karibuni yakionyesha mabadiliko chanya katika kikosi hicho
Mette aliyeajiriwa Februari ishirini mwaka elfu mbili ishirini na sita kuchukua nafasi ya Charles Okere ameshacheza mechi nane za Ligi Kuu Kenya akishinda nne akipoteza tatu na kutoka sare moja huku pia akiipeleka Tusker hadi robo fainali ya Kombe la FKF
Kocha huyo mwenye leseni ya UEFA Pro amesema timu imepanda kutoka nafasi ya kumi hadi ya saba ikiwa na pointi arobaini na moja na ana imani inaweza kuendeleza mwendo huo katika ligi na michuano ya kombe kuelekea msimu ujao.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































