JUVENTUS YAMNYATIA ALISSON KAMA LENGO KUU
Klabu ya Juventus inapanga kusajili kipa wa kiwango cha juu katika dirisha la usajili wa majira ya kiangazi huku Alisson Becker akitajwa kuwa chaguo lao kuu
Licha ya Liverpool kuongeza mkataba wa kipa huyo hadi mwaka 2027 mazungumzo yanatarajiwa kufanyika kati ya pande husika pamoja na kambi ya kipa Giorgi Mamardashvili katika wiki zijazo
Inaelezwa kuwa Alisson anapendezwa na wazo la kurejea Italia lakini bado ana heshima kubwa kwa klabu ya Liverpool hali inayoweza kufanya maamuzi yake kuwa ya tahadhari katika hatua zijazo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































