UPINZANI WATISHIA KUMREJESHA RAIS RUTO ICC
Hulka ya matumizi ya magenge ya wahuni kuvuruga mikutano ya kisiasa imechukua mkondo mpya, muungano wa upinzani sasa ukitishia kuishtaki serikali ya Rais William Ruto katika mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu, ICC.
Viongozi wa muungano huo akiwemo Kalonzo Musyoka wa Wiper na Rigathi Gachagua wa DCP, wamedai kuwa magenge hayo yanafanya kazi kwa ushirikiano na idara ya polisi kutatiza mikutano ya wanaopinga serikali.
Wameilaumu wizara ya usalama wa ndani kwa kutokana na hulka hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































