MASENETA WAITIA IPOA KIKAANGONI
Mamlaka ya kutathmini mienendo ya maafisa wa polisi, IPOA, imejipata chini ya darubini ya maseneta kuhusiana na utendakazi wake, maseneta wakiitaka kuweka wazi hatua zilizopigwa katika kuchunguza visa vya mauaji ya raia vinavyowahusisha polisi.
Katika kikao cha kujadili hoja ya seneta wa Embu Alexander Mundigi kuhusiana na mauaji ya watu 3 wakati wa maandamano dhidi ya hospitali ya Ishiara Level 4, maseneta wametilia shaka uwezo wa IPOA kuwachunguza polisi, wakipendekeza kuvunjiliwa kwake.
Wamekosoa hatua ya utoaji wa fidia kugharamia mienendo ya polisi kutumia nguvu kupita kiasi.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































