ODM-UDA WAZIKA TOFAUTI KUDUMISHA USHIRIKIANO
Vyama vya ODM na UDA vimekubali kuzika tofauti za kisiasa zilizokuwa zimeanza kujitokeza katika siku za hivi punde, vikiahidi kushirikiana na kuunga azma ya Rais William Ruto kuchaguliwa kwa muhula wa pili.
Katika mkutano ulioandaliwa katika Ikulu ya Nairobi, vyama hivyo vimewaagiza wenyekiti wake kuendelea na mazungumzo, kwa lengo la kuweka msingi wa masuala muhimu yatakayoongoza ushiriikiano huo.
Aidha, kamati maalumu ya ushirikiano itabuniwa ikiwajumuisha vinara wa vyama hivyo, mawaziri kadhaa, na viongozi wa walio wengi na wachache katika mabunge yote mawili kwa lengo la kuhakikisha utekelezaji wa ajenda ya serikali.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































