#Sports #Volleyball

KCB WAPEPETWA NA AL AHLY FAINALI YA VOLIBOLI

Matumaini ya klabu ya voliboli ya KCB kunyakua tena ubingwa wa voliboli katika mashindano ya wanawake barani Afrika yaliyeyushwa baada ya kupepetwa seti 3-1 na Al Ahly ya Misri kwenye fainali ya mashindano hayo jana.

Mabingwa hao wa mwaka 2022 walitangaza ubabe wao na kushinda seti ya kwanza 25-22, ila wakashindwa kustahimili makombora ya miamba hao wa Misri katika seti zilizofuata, wakipoteza 15-25, 2025 na 14-25.

Ushindi huo uliwapa Al Ahly ubingwa wa mara 11 barani Afrika, wa jana ukiwa wa kwanza tangu mwaka 2019 baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Zamalek katika fainali 2 zilizopita.

Awali katika uwanja huo, mabingwa mara 6, Kenya Pipeline, waliwalaza De Carthage ya Tunisia seti 3-1 kumaliza katika nafasi ya 3.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *