#Football #Sports

YAMAL ATARAJIWA ‘KUWA SAWA’ KWA KOMBE LA DUNIA

Kinda wa Barcelona Lamine Yamal ameratibiwa kushiriki michezo ya kombe la dunia baadaye mwaka huu licha ya kuratibiwa kuwa nje ya kikosi cha Barcelona kwa kipindi kilichosalia msimu huu kutokana na jeraha.

Yamal mwenye umri wa miaka 18 alipata jeraha la msuli katika mechi ya Jumatano dhidi ya Celta Vigo ambapo Barca walipata ushindi wa bao 1-0

Bao hilo lilifungwa na Yamal kupitia mkwaju wa penalty katika dakika ya 40 kabla yake kuashiria kwa madaktari kwamba alikuwa na tatizo.

Kwenye taarifa, Barca ilithibitisha jana kwamba atakosa kipindi kilichosalia kwa msimu.

Uhispania wataanza kampeni yao ya kombe la dunia dhidi ya Cape Verde Juni 15, kabla ya Saudi Arabia na kisha kukamilisha mechi za Group H dhidi ya Uruguay.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *